Haruna Moshi kurejeshwa Taifa Stars
Kwani Poulsen aliweza kuwaita washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas
Ulimwengu, wanaoichezea Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo.
Mbali na hilo Kiungo Mshambuliaji wa Simba Haruna Moshi 'Boban', ni
miongoni mwa majina 25 ya kikosi yaliyoanikwa na Kocha wa Timu ya Soka
ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Kim Poulsen kinachojiandaa kwa
mchezo wa kufuzu kwa fainali z Mataifa ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Kocha huyo aliweza kumtema Nahodha wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa
wakiwemo na viungo wengine Nadir Haroub ‘Canavaro’ wote kutoka Yanga,
Henry Joseph wa Kongsivinger ya Norway, Danny Mrwanda wa DT Long
An ya Vietnam na kiungo aliyefungashiwa virago na timu ya Philadephia Nizar Khalfan.
Alisema kikosi hicho kitaingia kambini kesho hapa Jijini, na uteuzi
wake uwezingatia uwezo wa mchezaji kwa nafasi anayochezea na uwiano
kwenye nafasi zote ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Akitetea uamuzi wake wa kumrudisha kwenye kikosi cha timu hiyo kiungo
mwenye rekodi ya utovu wa nidhamu Boban, alisema kuwa anampa nafasi
nyingine mchezaji huyo kwani ameonesha uwezo mkubwa kwenye timu yake ya
Simba msimu huu.
Mbali na kiungo huyo kurejeshwa pia alimrejesha mfungaji bora wa Ligi
Kuu John Bocco wa Azam, aliyetangaza kustaafu soka la Kimataifa
kutokana na kuzomewa mara kwa mara na mashabiki kila anapoichezea timu
ya taifa.
Alisema kuwa amemuita mshambuliaji huyo baada ya kuzungumza naye na kufanikiwa kumshawishi kubadili uamuzi wake.
Amemuacha Nahodha Nsajigwa kutokana na kuwa kwenye kiwango cha chini
kwa sasa na timu yake ya Yanga, kuwa kwenye msimu mbaya, sababu ambayo
pia ameielezea kwa Canavarro.
Kuhusu kuacha wachezaji wanaocheza nje ya nchi alisema wachezaji hao
wana viwango sawa na wachezaji wanaocheza soka hapa nyumbani na kwamba
wanatakiwa kuwa na viwango vya juu kuliko vya nyota wanaocheza ndani.
Kim pia amewajumuisha kwenye kikosi chake wachezaji kadhaa wa timu ya
Taifa ya Vijana na chipukizi toka Simba, ambao ni Simon Msuva (Moro
United- U20), Frank Domayo (JKT Ruvu- U 20), Edward Christopher (Simba),
Jonas Mkude (Simba-U 20) na Ramadhani Singano (Simba-U 20).
Kikosi kamili cha timu hiyo kinaundwa na makipa: Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar).
Mabeki ni Nassor Masoud ‘Cholo’ (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir
Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri
Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin
Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar),
Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo
(JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20),
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna
Moshi ‘Boban’ (Simba) na John Bocco (Azam).
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 dhidi ya Malawi
kabla ya kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 jijini Abidjan.
0 comments:
Post a Comment