Katika kuhakikisha kuwa tunakwenda na kasi ya teknologia inayoenda
kwa kasi duniani, Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) sasa kimeanza rasmi
kufundisha kwa kutumia mtandao na kuhakikisha
kila mhadhiri, anafundisha madenti wengi kwa wakati mmoja.
Hilo liliwekwa wazi juzi na Balozi Juma Mwapachu, alipokuwa
akizungumza na wahadhiri wa Udom katika ufunguzi wa mafunzo ya
ufundishaji kwa njia ya teknolojia hiyo.
Mwapacha ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la chuo hicho, alisema
wingi wa wanafunzi katika chuo hicho kikubwa kwa sasa hauendani na idadi
ya wahadhiri waliopo na kwamba bila ya kuwa na mbinu mbadala za
kuwafundisha, wanafunzi wataachwa nyuma.
“Udom sio chuo cha kawaida katika nchi za Afrika Mashariki, lakini
pia niseme kuwa siyo vyuo vingi hapa duniani vimeweza kupata bahati ya
kukua kwa kasi kubwa ndani ya miaka minne kama Udom, kwa hiyo ukuaji wa
chuo hiki lazima uwe wa kisasa na unaokwenda na sayansi na teknolijia,”
alisema
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Udom, Prof Idris Kikula, alisema chuo
kilikuwa kinakabiliwa na tatizo katika ufundishaji, hatua
iliyoulazimisha uongozi kubuni mkakati huo.Kikula alisema hatua ya sasa
ni ya kuwajengea uwezo wahadhiri, ili waweze kufanyakazi zao kwa ufanisi
mkubwa zaidi.
Home »
» UDOM sasa kufundisha kwa MTANDAO!
UDOM sasa kufundisha kwa MTANDAO!
Written By mahamoud on Tuesday, May 15, 2012 | 1:21 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment