Kama nchi, Tanzania imesaidiwa kwa kiasi
kikubwa na Marekani kupitia miradi mbalimbali
Watanzania wanasubiri kwa hamu ujio wa Rais Barrack
Obama kuwa utakuwa ni neema katika harakati za kujiletea maendeleo.
Ni heshima kubwa kama taifa kupokea ugeni mzito wa
kiongozi wa dola lenye nguvu zaidi duniani.
Kumbuka mwezi Machi Tanzania ilipokea ugeni wa Rais Xi
Jinping wa China, ambayo katika siku za karibuni imekuwa na nguvu za kutisha
katika medani ya uchumi duniani.
China ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania,
lakini katika miaka ya karibuni Marekani imetoa fedha nyingi za misaada na
kuanzisha miradi mikubwa ya kuisaidia Tanzania.
Marekani ni kati ya washirika wakubwa wa maendeleo kwa
Tanzania kwani katika mwaka 2012 ilimwaga misaada yenye thamani ya
Dola750 milioni (Sh1.2 trilioni) kusaidia shughuli za maendeleo.
Nchi hiyo kupitia mfuko wa Global Fund imekuwa
ikigharamia kampeni za kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu na
Malaria.
Global Fund inafanya kazi kwa kushirikiana na Shirika la
Afya Duniani (WHO) na Umoja wa Mataifa (UN).
Pia, kuna miradi mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji,
elimu, ulinzi na masuala ya ushauri katika usimamizi wa fedha. Shirika la
Maendeleo la Marekani (Usaid) lilitoa Dola 350 milioni (Sh558 bilioni)
kwa mwaka 2012 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Pia, limemwaga kiasi kingine cha Dola10.5 milioni (Sh16
bilioni) kwa ajili ya ujenzi wa sehemu za kuhifadhia dawa kwa Tanzania Bara na
Zanzibar.
Usaid, pia imekuwa ikisaidia katika harakati za kuinua
uelewa wa kinamama katika kutambua haki zao. Tayari, watu wapatao 23,000
wamenufaika kutokana na mpango huo.
SHIRIKA LA MILLENIUM CHALLENGE-MCC
Katika kipindi cha miaka mitano, shirika hili limetoa
kiasi cha Dola 698 (Sh1.1 trilioni) ili kusaidia katika kuimarisha sekta za
usafiri, nishati na maji.
Pia, Serikali ya Marekani imekuwa ikisaidia katika
kuka-mbana na rushwa na hasa katika masuala ya manunuzi. Pia imekuwa ikitoa
misaada mingi kwa Taasisi ya Kupambana na Kukabiliwa na Rushwa (Takukuru).
MRADI WA FEED THE FUTURE (FTF)
Serikali ya Marekani inaunga mkono Programu ya Tanzania
ya kuinua kilimo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ili kujenga uwezo wa
kujitosheleza kwa chakula.
Inagharamia mpango huo kupitia mradi wa Feed the Future,
ambao unafadhiliwa na ofisi ya Rais wa Marekani.
Asilimia 80 ya fedha za taasisi hiyo zinagharamia mpango
wa Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT). Mpango huo una
lengo wa kupandisha kilimo katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Iringa na Rukwa.
MPANGO WA PARTNERSHIP FOR GROWTH
Rais Barrack Obama ameanzisha mpango wenye jina la
`Partnership for Growth’ wenye lengo la kukabiliana na changamoto
zinazokwamisha uchumi wa Tanzania kukua. Changamoto hizo kama zime za umeme na
matatizo ya miundo mbinu.
MRADI WA PEPFAR
Mradi unaoitwa President’s Global Health
Initiative (PEPFAR) unaendesha kampeni kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa
Ukimwi. Tangu mwaka 2004, Tanzania imepokea Dola2.2 bilioni (Sh3.5 trilioni)
kutoka taasisi hii.
Pia, inaunga mkono kampeni ya kuhamasisha watu kupima
ili kufahamu kama wana ugonjwa wa Ukimwi.
MALARIA INITIATIVE (PMI)
Mpango huu unasimamiwa na Serikali ya Marekani na ndio
kwa kiasi kikubwa unasaidia kampeni ya kukabiliana ugonjwa wa Malaria nchini
Tanzania. Mradi huu umesaidia kusambaza vyandaruai milioni sita kwa
wanawake na watoto. Kampeni hii imesaidia kushusha maambukizi ya malaria kwa
asilimia 45 kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano.
PEACE CORPS
Serikali ya Marekani imekuwa ikileta wafanyakazi wa
kujitolea hasa katika sekta ya elimu tangu mwaka 1962. Wafanyakazi hao kupitia
mpango unaoitwa Peace Corps Volunteers. Wafanyakazi hao wa kujitolea huja kwa
ajili ya kusaidia katika sekta za elimu na afya. Walimu wa wanaokuja nchini
huwa zaidi wa maomo ya sayansi na hisabati. Wakati wengine husaidia sekta ya
afya.
USHIRIKIANO WA SEKTA YA ULINZI
Wanajeshi wa Marekani hutumwa nchini kufanya kazi za
kujitolea kama zile za kuchimba visima, kujenga shule na zahanati.
Pia , nchi hiyo hutoa mafunzo kwa majeshi ya
Tanzania ili wafanye kazi kwa ufansi kwenye kazi za kulinda amani. Tanzania
hivi sasa ina majeshi katika nchi za Lebanon, Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo, DRC.
Halikadhalika. Wamarekani hufundisha wanajeshi na
polisi wa Tanzania. Kuanzia askalit 15-20 hupata mafunzo kila mwaka nchini
Marekani.
BENKI KUU YA TANZANIA
Marekani imeweka mtaalamu wake katika Wizara ya Fedha
ili kushauri namna nzuri ya ulipaji madeni ya Tanzania. Mtaalamu huyo anfanya
kazi na Wizara na Benki Kuu (BoT).
KUBADILISHANA UZOEFU
Pia, Watanzania wapatao 20 kila mwaka huwa wananufaika
na Marekani katika mpango wa kubadilishana wanafunzi na wataalamu. Mpango huu
umenufaisha watu kutoka Bara na Zanzibar. Wanafunzi na wasanii wa Tanzania
wamepata nafasi ya kuzuru Marekani kushiriki katika matamasha mbalimbali huko.
MIFUKO MINGINE
Pia, kuna mifuko mbalimbali, ambayo inasaidia maendeleo
ya Watanzania kama ule wa Mfuko wa Balozi wa Marekani wa Kulinda vivutio vya
Utamaduni, pia kuna Mfuko wa Kukabiliana na tatizo la Uhamiaji Haramu na
mwingine kwa ajili ya kushughulikia masuala ya demokarisa Haki za Binadamu.
Mifuko yote imetoa mamilioni ya fedha, ambayo Watanzania
wamenufaika nayo.
CHANZO: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment